Bishop Dr. Jangalason - Usiku Mtakatifu (Wimbo Wa Christmas)
0
0
1 Visualizzazioni·
01 Agosto 2023
In
Sermons
LYRICS USIKU MTAKATIFU
Usiku Mtakatifu, Holini mwa ng’ombe,
Amezaliwa Mtoto ndiye Imanueli.
Yesu Bwana, Mwana wa Mungu,
ni shangwe ya Dunia, Yesu Amezaliwa.
Mji ule wa Daudi, Furaha Bethlehemu,
Mungu amevaa mwili, Amekuja kwetu.
Imanueli, Mungu pamoja nasi,
hii ni neema kuu, Yesu Amezaliwa.
Malaika wanaimba Utukufu mbinguni,
na duniani amani, Mungu Amekuja,
Ni upendo gani!, Mungu kutujia sisi,
Tuimbe halleluya, Yesu amezaliwa.
Karibu, Bwana Yesu, ingia moyoni mwangu,
unibadilishe, nifanane na Wewe
Mawazo ya moyo wangu,
Maneno ya kinywa changu,
yaongozwe N awe, Ewe Mungu wangu!
Bishop Dr. Jangalason © 2021
#UsikuMtakatifu#CharlesJangalason#
Mostra di più
0 Commenti
sort Ordina per